Thursday, 8 February 2018

Usalama bado ni mtihani mkuu kwa utawala wa Somalia.


Rais FarmaajoHaki miliki ya pich
Image captionRais Mohamed Abdullahi Farmaajo
Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi al maarufu Farmaajo hii leo amefikisha mwaka mmoja tangu achaguliwe.
Mtihani wake mkubwa ungali ni hali ya usalama, huku wapiganaji wakiendelea kufanikisha mashambulio jijini Mogadishu na kwingineko nchini.
Mwezi mitano tu iliyopita, mlipuko wa bomu ya lori iliwaua watu wasiopungua mia tano, kwenye shambulio lilokuwa hatari zaidi katika historia ya nchi hiyo.
Kwenye makutano ya barabara katika soko la Zoobe jijini Mogadishu, biashara imenoga huku na kule. Lakini wengi wa wachuuzi na wauzaji hapa ni waathiriwa wa mkasa wa bomu uliokuwa hatari zaidi katika historia.
Mmoja wao ni Abdifittah Ahmed, mwenye umri wa miaka 28 na na anayemiliki duka la dawa. Uso wake una makovu mawili; moja unapunda kovu la uso wake, linguine linaanzia mdomoni hadi chini ya sikio lake la kushoto. Huku tukitembea barabarani, anakumbuka jinsi alivyojikokota kutoka vifusi vya duka lake.
Abdifittah Ahmed
Image captionAbdifittah Ahmed
Bomu hilo iliporomosha jumba la gorofa mbili alimokuwa akifanyia mauzo.
'Niliivuka barabara hii nikiwa natokwa na damu kichwani, niliiona miili ya watu ikiwa imezagaa barabarani, wengi wakiwa na majeraha, wengine wamepoteza sehemu zao za mwili, wengine wamepoteza fahamu.
'Sikuweza kuona vizuri kwasbabu damu ilikuwa inatiririka kutoka machoni mwangu, lakini bado naona nilikuwa na bahati, kwasababu nilichokiona ilikuwa hali mbaya mno', amesema Abdifittah
Mwanaume mmoja akihuzunika karibu na maiti katika eneo ambapo bomu lililipukia jijini Mogadishu Oktoba 14, 2017Haki miliki ya picha
Image captionMwanaume mmoja akihuzunika karibu na maiti katika eneo ambapo bomu lililipukia jijini Mogadishu Oktoba 14, 2017
Aliwapoteza marafiki wengi siku hiyo. Uharibifu uliosababishwa na mlipuko huo ulienea kwa mamia ya hatua, na kuwaacha wengi wakiwa wamekufa au kujeruhiwa.
Kwa sasa ni vigumu kutambua yaliotokea katika enoe hilo unapotembea. Huwezi kutambua kwamba hapa ndipo watu wengi walipoteza maisha yao miezi mitano iliyopita.
Majengo mengi yamejengwa upya, barabara imetengenezwa, na wafanyabiashara wanaendelea na shughulia zao kama kawaida.
Kikosi maalumu cha jeshi kimeimarisha ukaguzi wa magari haswa nyakati za jioni Mogadishu
Image captionKikosi maalumu cha jeshi kimeimarisha ukaguzi wa magari haswa nyakati za jioni
Watu wameamua kuendelea na maisha yao kana kwamba hakuna kilichotokea. Lakini akilini mwao shambulio hilo limewacha kovu na kumbukumbu zitakazodumu maisha.
Miezi michache baada ya kutwaa urais wa Somalia kutoka uwanja wa ndege kwa kuhofia mashambulio ya Al Shabaab, Mohamed Abdullahi alitoa ahadi yake kwa wananchi wa Somalia.
Alisema, 'Lengo langu ni kuwashinda Al Shabaab kwa miaka miwili ijayo. Natumai kwamba tukifanya kazi pamoja, tutaleta Amani na utulivu nchini Somalia'.
Lakini uongozi wake umeshuhudia mashambulio, na Mogadishu ingali mojawapo wa miji hatari zaidi duniani.
ramani
Wachanganuzi wanaamiini kuwa jinamizi la Al Shabab ni gumu kuliangamiza..
Hassan Sheikh, ni mchambuzi wa masuala ya usalama anasema, 'Kwa sababu ni wapiganaji, wanaweza kupenya kirahisi katika maeneo ya umma na ya kibinafsi, na wana athari kubwa katika mfumo wa jamii kisiasa, kiuchumi na kijamii.
'Muhimu zaidi ni kuwa walisababisha uoga, na uoga huu huwasaidia kwani ni vigumu sana kuwakamata au kuwashinda'.
Mapema wiki hii, mahakama kuu ya Somalia ilimpata na hatia mshukiwa mmoja wa mashambulio hayo na kumhukumu kifo, huku mwengine ambaye hakuwa mahakamani akihukumiwa kifungo cha maisha.
Barabarani, kikosi maalumu cha jeshi kimeimarisha ukaguzi wa magari haswa nyakati za jioni; huku magari karibu yote yakisimamishwa na kukaguliwa vikali pamoja na abiria.
Wakazi wanatumai kwamba hatua hizi zitaweza kurejesha matumaini yao ambayo kwa sasa yako gizani.
Chanzo:Bbc swahili
#Changia Damu Okoa Taifa

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...