Mtu
mmoja aliyekuwa akijulikana kwa jina la Hassan Damsoni mkazi wa kijiji cha
Katambike kata ya Ugalla Mkoani Katavi ameuawa na watu wanaodhaniwa kuwa ni
majambazi.
Kwa
mjibu wa diwani wa kata hiyo Mh.Halawa Malembeja amesema kuwa tukio hilo
limetokea usiku wa January 27 majira ya saa tano usiku ambapo mbali na kuuwawa
kwa mkazi huyo watu hao wamepora zaidi ya shilingi milioni mbili kutoka nyumba
tano na kujeruhi wengine.
Kwa
mjibu wa Diwani Malembeja mazishi ya marehemu yamekwishafanyika katika kijiji
hicho huku akieleza kuwa wananchi wamesikitishwa na tukio hilo na kuliomba
jeshi la polisi kupeleka kituo cha polisi katika kata hiyo kwa ajili ya
usalama.
Kwa
upande wake kamanda wa Polisi Mkoani Katavi ACP Damasi Nyanda amekiri kutokea
kwa tukio hilo na amesema wamemkamata mtu mmoja akiwa na silaha aina ya gobole
na simu tano ambazo zilikuwa zimeondolewa.
Hata
hiyo Jeshi la polisi limetoa wito kwa watu kuacha kujihusisha na uharifu kwani
kufanya hivyo ni kosa kisheria ambapo msako unaendelea ili kuwakamata wahusika
wa tukio hilo ili wafikishwe katika vyombo vya sheria.
Chanzo:Issack Gerald
#Changia Damu Okoa Maisha
No comments:
Post a Comment