Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Moshi imewasomea shitaka la mauaji watu watatu wanaotuhumiwa kumuua kijana Humphrey Makundi aliyekuwa mwanafunzi wa kidato cha pili.
Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini
Moshi imewasomea shitaka la mauaji watu watatu wanaotuhumiwa kumuua kijana
Humphrey Makundi aliyekuwa mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya
Sekondari ya Scolastica iliyopo Moshi.
Watuhumiwa hao ni mmiliki wa shule ya Scolastica, Edward Shayo mwenye
miaka 63, mlinzi wa shule hiyo Hamis Chacha mwenye miaka 28 na Laban Nabiswa
mwenye miaka 37.
Upande wa Jamhuri katika shitaka hilo lililofika mbele ya Hakimu Mkazi,
Julieti Mawore umewakilishwa na Mwanasheria Kassim Nassiri akisaidiana na
Wakili wa kujitegemea, Faygrace Sadallah.
Akisoma maelezo ya hati ya mashitaka mbele ya mahakama hiyo, Nassiri ameeleza kuwa mnamo Novemba 6 mwaka
huu mshitakiwa wa kwanza, Hamis Chacha wa pili Edward Shayo na wa tatu Laban
Nabiswa, walimuua kwa kukusudia mtu aitwaye Humphrey Makundi.
Hakimu Mkazi Mawore, ameahirisha shitaka hadi Desemba 8 mwaka
huu litakapotajwa tena na kwamba washitakiwa wote watarudishwa
rumande kutokana na kesi hiyo kutokuwa na dhamana.
No comments:
Post a Comment