Tuesday, 28 November 2017

Serikali imeshauriwa kuweka mazingira mazuri kwa sekta ya mifugo ili kuongeza uzalishaji wa bidhaa zinazotokana na mifugo.




Serikali imeshauriwa kuweka mazingira mazuri kwa sekta ya mifugo ili kuongeza uzalishaji wa bidhaa zinazotokana na mifugo.

Wadau wa sekta hiyo wamesema hilo litawezesha azma ya Serikali ya kuwa na uchumi wa kati utokanao na viwanda kufikiwa.

Wamesema hayo leo wakati wa uzinduzi wa mkakati wa ushawishi wa sera ya mifugo ulioandaliwa na jukwaa la wadau wa kilimo (Ansaf).

Katibu mkuu wa chama cha wafugaji nchini, Magembe Makoye amesema kuhamahama wafugaji kunasababisha ufugaji usio na tija na manufaa kwa viwanda, hivyo sekta hiyo kuendelea kuendeshwa kwa mazoea.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk Maria Mashingo amesema wakati umefika  kwa wafugaji kuacha kufuga kwa mazoea na kuangalia zaidi biashara.

 CHANZO: HABARI LEO.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...