Tuesday, 28 November 2017

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imesema Taratibu za kisheria zinachelewesha kuwasilisha kesi Mahakama ya Mafisadi.




 

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imesema Taratibu za kisheria zinachelewesha kuwasilisha kesi Mahakama  ya Mafisadi.

Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya maadili, Mlowola amesema kuna kesi ambazo ziko tayari kuanza kusikilizwa, lakini kuna utaratibu wa kisheria uliopo ambapo kabla ya kwenda kwenye mahakama hiyo ni lazima kupita katika taratibu hizo.

Mlowola amesema kesi hizo zitasikilizwa na Mahakama ya Rushwa na Ufisadi, lakini kinachochelewesha kwa sasa ni sababu za kiufundi za mahakama hiyo ambazo bado wataalamu wanazishughulikia.

Hata hivyo, tayari mahakama hiyo imeshaanza kazi na mashauri kadhaa yameanza kushughulikiwa na mahakama hiyo.

CHANZO: MWANANCHI

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...