Tuesday, 28 November 2017

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amefanya ziara katika bandari ya Dar es salaam.



Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amefanya ziara katika bandari ya Dar es salaam, ili kufanya ukaguzi wa magari 31 ya Jeshi hilo ambayo Mhe. John Pombe Magufuli, alielekeza kukabidhiwa kwa Jeshi hilo ili kurahisisha utendaji kazi

Akiwa Bandarini IGP Sirro amekutana na kufanya mazungumzo na askari wa Jeshi hilo Kikosi cha Bandari ambapo amewataka kuhakikisha wanatimiza majukumu ipasavyo pamoja na kutenda kwa wateja.

Hata hivyo IGP amewataka Polisi wasaidizi wanaofanya kazi bandarini hapo kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kuendelea kudhibiti vitendo vya kihalifu vinavyofanywa na baadhi ya watu wasio waaminifu.

CHANZO: MWANANCHI

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...