Na Mdaki Husein
Chama Cha Mapinduzi CCM
Mkoa wa Katavi kesho kinatarajia kufanya uchaguzi wa kuwapata viongozi wa
nafasi za jumuiya mbalimbali Watakaoongoza jumuiya hizo kwa miaka mitano ijayo.
Akizungumza na Mpanda
Redio Katibu wa Chama hicho Mkoa wa Katavi Bw. Kajoro Vyohoroka amewataka
wagombea wa nafasi zote za jumuiya za chama kufuata kanuni za uchaguzi.
Amesema wagombea wote
wanapaswa Kufanya za kampeni kistaarabu na kuacha vitendo vya Rushwa na kusema
kuwa mgombea atakayebainika ameshinda kwa kutoa rushwa atafutiwa matokeo yake.
Katika hatua nyingine
Katibu huyo amesema baada ya uchaguzi huo wa jumuiya za vyama hapo kesho
wanatarajia kufanya uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi ngazi ya mkoa kufanyika
tarehe 5 mwezi wa 12 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment