Sunday, 9 July 2017
KIONGOZI WA UPINZANI LEOPOLDO LOPEZ AACHILIWA VENEZUELA.
Bwana Lopez (juu) akishagiliwa na wafuasi wake mjini Caracas
Rais wa Venezuela Nicolás Maduro amepongeza hatua ya kumuachilia kutoka gerezani moja wa viongozi wakuu wa upanzani nchini humo Leopoldo Lopez. Bwana Lopez amepelekwa katika kifungo cha nyumbani baada ya kukaa gereza kwa zaidi ya miaka mitatu. Maandamano yasababisha vifo Venezuela na Maandamano yaendelea Venezuela Aliondoka gerezani karibu na mji wa Caracas na kujiunga na familia yake siku ya Jumamos tarehe 8 mwezi huu. Bwana Lopez alikuwa akitumikia kifungo cha miaka 14 kwa kuchochea ghasia wakati wa maandamano ya kuipinga serikali mwaka 2014, mashtaka ambayo ameyakanusha. Mahakama kuu inasema kuwa ameachiliwa kwa misingi ya kiafya.
kiongozi wa upinzani Leopoldo Lopez kuwakumbatia his watoto wake nyumban kwake Caracas baaada ya kuachiwa kutoka kifungonifrom Lopez akiwa na watoto wake.
Bwana Maduro alisema kuwa anaunga mkono na kuheshimu uamuzi wa mahakama lakini lakini akataka kuwepo kwa amani. Saa chacahe baada ya kuichiliwa Bwana Lopez aliwashauri wafuasia wake kuendelea kuandamana barabarani kumpinga Bwana Maduro.
Wanajeshi kukabiliana na maandamano Venezuela Waandamanaji zaidi wameuwawa Venezuela Akielezea maisha ya mwawawe gerezani babake Lopez aliiambia radio moja ya Uhispania siku chache zilizopita kuwa aliadhibiwa kwa kufungiwa katika chumba kisicho na mwangaza na maji kwa muda wa siku tatu. Alisema kuwa mwamawe sasa alikuwa amefungiwa kifaa cha eletroniki ili mamlaka ziwezi kufuatilia mienendo yake. kiongozi wa upinzani wa Venezuela Leopoldo Lopez akionesha bendela ya nchi ya Venezuela akiwasalimu wanaomuunga mkono njee ya nyumbani kwake Caracas.
Lopez alipigwa picha akishika bendera ya Venezuela.
habari kutoka Bbc swahili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Featured post
MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO
Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio ...
-
NSIMBO Soko la Katumba Mnyaki linalomilikiwa na halamshauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi halina choo tangu kuanzishwa kwake hali...
-
MLELE Shule ya msingi kusa iliyopo katika kijiji cha Kanoge kata ya utende Halmashauri ya wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi inatalajia k...
-
Imeandikwa na. Prosper Kwigize, Kasulu, Kigoma Sisi vijana wenye vipaji tupo wengi sana vijijini, elimu yetu ni ya darasa la saba laki...
No comments:
Post a Comment