NSIMBO
Baadhi ya wanufaika wa
mpango wa kunusuru kaya maskini Tasaf katika kijiji cha Mtapenda Halmashauri ya
Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi,wameishukuru tasaf kwa kuwawezesha kujikwamua
kimaisha.
Wanufaika hao wametoa shukurani hizo mbele ya vyombo vya habari mara baada ya kutembelewa na Tasaf ili kukagua namna wanavyotumia ruzuku wanazopewa
Wakati huo huo wamewashauri
wanufaika wenzao kutumia vizuri ruzuku wanazopewa ili kutatua changamoto
mbalimbali zinazowakabili ikiwemo kuboresha makazi yao.
Mradi wa tasaf katika
Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ulianza kutekelezwa mwaka 2015 ili kuainisha
kaya maskini zinazotakiwa kupewa ruzuku ili kujinusuru na umaskini ambapo tangu
mwaka jana vijiji saba vimenufaika.
Chanzo:Mpanda Radio
No comments:
Post a Comment