Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge wanawake TWPG, Bi. Magreth Sitta
DAR ES SALAAM
Mwenyekiti wa Chama cha
Wabunge wanawake TWPG, Bi. Magreth Sitta ameitaka serikali kuandaa mazingira na
miundombinu itakaowasaidia watoto wa kike kupata elimu bila kukatisha masomo
wanapokuwa katika kipindi cha hedhi.
Mwenyekiti huyo wa TWPG
amesema hayo katika Mafunzo maalumu ya baadhi ya wabunge walioteuliwa juu ya
hedhi salama kwa watoto wa kike ambapo wabunge hao wametunikiwa ubalozi kuhusu
elimu hiyo.
Bi Magreth Sitta amesema kuwa
serikali ina wajibu wa kipekee katika kufikisha elimu kwa watoto wa kike huku
wabunge wangine wakimuunga mkono juu ya jitihada za serikali katika kufanikisha
azma hiyo.
Aidha wabunge mbalimbali wameunga
mkono hoja hiyo kwa kuitaka serikali iliangalie suala hili kwa undani kwani kwa
makadirio ya watoto wa kike kushindwa kwenda shuleni kwa mwaka mzima lazima
ufaulu wake utakuwa chini.
Wiki iliyopita Mbunge wa
kuteuliwa upendo Penneza alijaribu kupeleka hoja binafsi kuhusu wanafunzi wa
kike kupatiwa pedi lakini hoja hiyo haikufanikiwa kwani hoja hiyo ilikataliwa
kwa sababu yakuwa inavunja ibara ya 99 (2) ya Katiba.
Chanzo:Eatv
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment