Wednesday, 4 October 2017

Catalonia kutangaza uhuru 'siku chache zijazo'.

Catalan President Carles Puigdemont speaks at a news conference in Barcelona. Photo: 2 October 2017
Rais wa Catalonia Carles Puigdemont
Haki miliki ya pichaImage captio
Catalonia itatangaza uhuru wake kutoka Uhispania siku chache zinazokuja, kiongozi wa eneo hilo ameiambia BBC.
Katika mahojiano yake ya kwanza tangu ifanyike kura ya maoni siku ya Jumapili, Carles Puigdemont alisema kuwa serikali yake itachukua hatua mwishoni mwa wiki hii au mwanzoni mwa wiki ijayo.
Kwa upande wake mfalme wa Uhispania Felipe VI, amasema kuwa waandalizi wa kura hiyo walikiuka sheria.
A woman wrapped in a Catalan flag listens to Spain's King Felipe VI in a bar in Barcelona. Photo: 3 October 2017Haki miliki ya pi
Image captionMfalme Felipe VI akihutubia taifa akitaka kuwepo umoja
Amasema kuwa hali ya sasa nchini Uhispania sio nzuri na kutaka kuwepo umoja.
Maelfu ya watu kote eneo la Catalonia wamekuwa wakigoma kupinga ghasa za polisi wa Uhispania wakati wa kura, ambapo takriban watu 900 walijeruhwia.
Roadblock on Gran Via in central Barcelona, 3 Oct 17Haki miliki ya picha
Image captionKuzuizi cha barabarani huko Gran Via
Wakati ya kura hiyo takriban polisi 33 pia walijeruhiwa.
Wakati wa mahojiano na BBC rais wa Catalonia Carles Puigdemont, alisema kuwa serikali yake itachukua hatua mwishoni mwa wiki hii au mwanzo wa wiki ijayo.
Barcelona anti-police roadblock, 3 Oct 17Haki miliki ya picha
Image captionWaandamanaji walifunga barabata nje ya kituo cha polis huko Barcelona
Alipoulizwa kuhusu ni kipi atakifanya ikiwa serikali ya Uhispania itaingilia kati na kuchukua udhibiti wa serikali ya Catalonia, Bw Puigdemont alisema kuwa yatakuwa ni makosa ambayo yatabadilisha kila kitu.
Barcelona metro, 3 Oct 17Haki miliki ya pichaEPA
Image captionKituo cha treni Barcelona
Bwana Puigdemont alisema kuwa sasa hakuna mawasiliano kati ya serikali mjini Madrrid na utawala wake.
Alipinga taarifa ya tume ya ulaya ya siku ya Jumatatu kuwa kile kinachoendelea Catalonia ni masuala ya ndania ya Uhispania.
Mercabarna market - outlets shut, 3 Oct 17Haki miliki ya pichaEPA
Image captionDuka kubwa la jumlahjuko Barcelona - Mercabarna - limetetizwa na mgomo
Catalonia

Monday, 2 October 2017

Waliokula mil 359/- za barabara zawakwama.


Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB), Joseph Haul
BODI ya Mfuko wa Barabara imeziamuru halmashauri saba nchini zilizotumia zaidi ya Sh milioni 359.5 zilizotolewa kwa ajili ya kujengea barabara, lakini zikazitumia kununua madawati na kujengea maabara kuzirudisha mara moja katika mfuko huo.
Halmashauri hizo ni Karagwe Sh milioni 55.5, Kyerwa Sh milioni 36.8, Ushetu Sh milioni 15.7, Masasi Mji Sh milioni 31.3, Nanyumbu Sh milioni 110.7, Kilolo Sh milioni 102.3 na Songea ya Mji Sh milioni 7.3, na zinatakiwa kurudishwa fedha hizo kabla ya Oktoba 30, mwaka huu. Hayo yalisemwa mjini Dodoma jana na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB), Joseph Haule wakati akiwasilisha taarifa ya ukaguzi wa kiufundi na fedha kwa kazi za ujenzi na matengenezo ya barabara na madaraja kwa mwaka wa fedha 2014/15 na 2015/16.
“Kwa zile halmashauri za wilaya zilizotumia fedha za Mfuko wa Barabara kwa matumizi mengine kama vile kutengenezea madawati na ujenzi wa maabara, wakaguzi wa halmashauri husika wahakikishe zinarudisha haraka katika akaunti ya Mfuko wa Barabara ya Dharura,” alisema Haule na kufafanua kuwa halmashauri hizo zilikiuka Sheria ya Fedha ya Mwaka 2001, Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2011 na Sheria ya Tozo za Barabara na Mafuta na Kanuni zake.
Pia kuna halmashauri ambazo zililipia jumla ya Sh milioni 87.1 kwenye kazi hewa ambazo hazijafanyika ambazo ni pamoja na Mtwara ambayo ililipa Sh milioni 46.2, Tanga Mjini Sh milioni 12.1, Monduli Sh milioni 6.6, na Moshi Sh milioni 12.2 nazo zinatakiwa kulipa fedha hizo. Halmashauri ya Gairo ambayo miradi mingi haijatekelezwa kadiri ya mikataba ya makubaliano, ilipewa nafasi ya kufika mbele ya Bodi ya Mfuko, lakini ilichelewa kufika.
“Halmashauri ya Kalambo, mkandarasi wake aliidhinisha malipo ya Sh milioni 15.4 ya kupima kifusi ambacho hakijashindiliwa kinyume cha mkataba unaotaka kuidhinisha malipo kifusi kilichoshindiliwa,” alisema na kubainisha kuwa Halmashauri ya Kakonko ilihamisha Sh milioni 13.7 zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya mradi wa matengenezo ya barabara na kutekelezea mradi mwingine, kinyume cha mkataba wa makubaliano. "Halmashauri ya Kondoa ilipewa zaidi ya Sh milioni 60 kwa ajili ya kujenga maeneo korofi na ikajenga chini ya kiwango na hivyo kuisababishia hasara kubwa serikali," alisema.
@habari na habari leo

Nkurunziza asifia bidhaa za Tanzania.



Rais wa Burundi  Pierre Nkurunziza. 

RAIS Pierre Nkurunziza wa Burundi ametembelea maonesho ya kwanza ya biashara ya Tanzania nchini Burundi yanayolenga kuangalia soko pana la bidhaa zinazotengenezwa na wajasiriamali kutoka Tanzania na kusifu ubora wa bidhaa hizo.
Maonesho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Tempete vilivyopo jijini Bujumbura, yalianza Septemba 28, mwaka huu na yalitarajiwa kukamilika jana, yameandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa lengo la kuongeza fursa za kibiashara katika nchi za ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati.
“Hii ni ishara ya kukomaa kwa udugu kati ya Tanzania na Burundi, wananchi wa Burundi walikuwa wakisafiri umbali mrefu kufuata bidhaa hadi Dar es Salaam, lakini sasa wameletewa mlangoni.
Kwa muda mrefu tumekuwa tukifurahia bidhaa aina hii, lakini bei zilikuwa kubwa kutokana na gharama za usafiri, kwa sasa mambo yamekuwa mazuri,” alisema Rais Nkurunziza. Rais Nkurunziza aliongeza kuwa: “Uhusiano wetu unazidi kuimarika, naamini ile dhana ya utangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki inatekelezwa kivitendo. Naahidi kuunga mkono juhudi zote za kuimarika kiuchumi kati ya nchi mbili hizi.”
Ubalozi wa Tanzania nchini Burundi kwa kiasi kikubwa umeshiriki kufanikisha maonesho haya chini ya Balozi Rajabu Gamaha ambaye ndiye aliyewashawishi maofisa wa TanTrade kuwa na maonesho aina hiyo kutokana na maombi ya kupata bidhaa kutoka Tanzania kuwa mengi ofisini kwake. Awali katika hotuba yake ya ufunguzi Septemba 27, mwaka huu, Makamu wa Pili wa Rais wa Burundi, Dk Joseph Bitore alisema biashara ni kitu kinachounganisha mataifa mawili kiuchumi hivyo watachukulia maonesho hayo kujifunza, lakini pia kutanua wigo wa mahusiano ya kiuchumi kati ya Tanzania na Burundi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TanTrade, Christopher Chiza alisema uamuzi wa kupeleka bidhaa Burundi ulipofika mezani kwake hakutaka kusita kwa sababu alijua hiyo ni njia pekee ya kufikisha mbali bidhaa za Kitanzania. “Tunapofanikiwa kufika Burundi maana yake tunalenga soko pana la ukanda huu, tunatarajia kufikia soko la Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa sababu hata wao tumearifiwa kuwa wananunua bidhaa kutoka Burundi,” alisema Chiza.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Edwin Rutageruka aliahidi kuendeleza biashara kati ya Tanzania na Burundi hata baada ya kumalizika kwa maonesho hayo. “Huu ni mwanzo, tayari wafanyabiashara tulioongozana nao wamechukua mawasiliano ya wateja wao na watawauliza wanahitaji nini ili walete.”

@habari na habari leo

Waomba kesi za mimba ziwe korti za mwanzo.


MWANASHERIA Grace Timoth ameiomba Serikali kuruhusu kesi zinazohusu mimba kwa wanafunzi, kuendeshwa na mahakama za mwanzo, badala ya mahakama za wilaya.
Amesema hali hiyo itawaondolea mzigo wazazi na mashahidi kufika kwenye mahakama za wilaya. Amesema kwa sasa watu wengi wamekuwa wakishindwa kufika wilayani, hali inayosababisha kesi nyingi kushindwa kupata ushahidi wa kutosha, hivyo watuhumiwa kuachiwa huru.
Timoth alitoa ombi hilo hivi karibuni wakati wa mafunzo kwa wenyeviti na wajumbe wa bodi za shule za sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro. Mafunzo hayo yaliandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali, inayojihusisha na masuala ya utawala bora ya Jikwamue Development Association (JIDA).
Mafunzo hayo yaliendeshwa kutokana na wilaya hiyo, kukabiliwa na tatizo la mimba, ambapo takwimu zinaonesha kuwa mwaka 2016/2017 wanafunzi 49 wamepata mimba. Mratibu wa Mradi wa Elimudira wa asasi ya JIDA, Shaban Chande alisema elimu itakayotolewa kwa wazazi kupitia mradi huo kwa ufadhili wa taasisi ya The Foundation For Civil Society kwa miezi sita, italeta hamasa ya uchangiaji chakula kwa wanafunzi shuleni.
Alisema elimu hiyo itahamasisha wazazi kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa na hosteli za kuishi wanafunzi hasa wa kike, badala ya kupanga mitaani, ambako wamekuwa wakikosa uangalizi wa wazazi.
@habari na habari leo

Daktari anayetuhumiwa kulewa yamkuta makubwa


WAZIRI wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu amemwelekeza Naibu Katibu Mkuu Tamisemi, Dk Zainab Chaula kumchukulia hatua daktari wa Hospitali ya Wilaya ya Maswa, Laurent Biyengo aliyedaiwa kushindwa kuingia kazini na kwenda kunywa pombe na kusababisha wagonjwa kutopatiwa huduma.
Aidha, Polisi wilayani humo imethibitisha kumkamata na kumseka ndani daktari huyo kwa maagizo ya Mkuu wa wilaya hiyo, Dk Seif Shekalaghe. Hatua imefikiwa baada ya baadhi ya wagonjwa waliofika katika hospitali hiyo Septemba 27, mwaka huu saa 1:00 hadi saa 3:30 usiku kukosa huduma kutokana na kutokuwepo kwa daktari huyo wa zamu na kusababisha ujauzito aliokuwa nao Salome John kutoka na kuharibika wakati akimsubiri daktari huyo aliyekwenda kulewa.
Waziri Ummy ametoa maelekezo hayo kwa njia ya simu baada ya kupata taarifa hizo kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) kutoka gazeti hili juu ya wagonjwa waliofika kupata huduma katika hospitali hiyo na kumkosa daktari wa zamu.
Wagonjwa waliopatwa na madhira hayo wakizungumza na waandishi wa habari katika Hospitali ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu walisema walifika asubuhi katika hospitali hiyo kwa ajili ya kupata matibabu, lakini cha kushangaza daktari wa zamu hakuwepo.
Walidai licha ya wauguzi kuwepo, lakini walishindwa kuwahudumia hasa mjamzito, Salome John aliyekuwa akilia kutokana na maumivu aliyokuwa akiyapata kwa maelekezo kuwa taratibu haziruhusu ni hadi hapo watakapoandikiwa cheti na daktari hali iliyosababisha mgonjwa huyo ujauzito wake kutoka.
“Nilimleta mwanangu akiwa ana mimba mara baada ya kunieleza ya kuwa anahisi maumivu makali tumbo tulifika hospitali majira ya saa 1:30 usiku, lakini daktari hatukumkuta licha ya kuandikiwa cheti lakini tulibaki kumsubiri daktari lakini hakuonekana ilipofika saa 3:20 usiku maumivu yalimzidi binti yangu na wauguzi walikataa kutuhudumia hadi tumwone daktari na hatimaye mimba yake ikatoka,” alidai Suzana Kalumbilo ambaye ni mama mzazi wa Salome.
Kwa mujibu wao, baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya kwa wagonjwa waliokuwepo walichukua jukumu la kumpigia simu Mkuu wa wilaya, Dk Shekalaghe ambaye naye alichukua jukumu la kumpigia simu Mganga Mkuu wa Wilaya, Dk Jonathan Budenu.
Walisema Dk Budenu aliyefika muda mfupi baada ya kupigiwa simu na DC wake, alifanya jitihada za kupata daktari mwingine ambaye alifika na kuanza kutoa huduma kwa wagonjwa waliokuwepo. Inaelezwa kwamba ilipofika saa 3:40 usiku ndipo Bihengo alipofika akiwa amelewa huku hajitambui na kuingia katika chumba cha daktari, lakini Mganga Mkuu wa Wilaya, Dk Budemu alimtoa na kumtaka asitoe huduma yoyote kutokana na hali aliyokuwa nayo.
@habari na habari leo

Upatikanaji takwimu waitatiza BoT


Baada ya ripoti ya tathmini ya uchumi kutotoka kwa miezi mitatu mfululizo, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema changamoto ya upatikanaji wa takwimu ndiyo sababu.
BoT hutoa ripoti hiyo kila mwezi ili kuwataarifu wadau wa uchumi na wananchi kwa ujumla mwenendo wa kiuchumi, lakini haijafanya hivyo kuanzia Juni hivyo kuibua maswali miongoni mwa wadau wanaozitumia taarifa hizo kwa shughuli zao.
Mkurugenzi wa Uchumi wa BoT, Johnson Nyela alisema maandalizi ya kukamilisha ripoti hizo yanaendelea kwa kuzishughulikia changamoto zilizopo.
“Nia yetu haiendani na hali halisi. Tungependa ripoti ya Januari kwa mfano itoke mwishoni mwa mwezi huo lakini hali halisi ni tofauti. Upatikanaji wa taarifa unasumbua,” alisema mkurugenzi huyo.
Nyela alisema taarifa ya Juni inakamilishwa na muda wowote itatoka wakati ile ya Julai bado inaandaliwa.
Ripoti hiyo ya kila mwezi huwekwa kwenye tovuti ya BoT ama mwishoni mwa wiki ya pili au mwanzoni mwa wiki ya tatu ya mwezi unaofuata, yaani ripoti ya Januari inawekwa muda huo Februari.
Lakini ripoti ya mwisho iliyopo kwenye tovuti ya BoT iliwekwa Juni ikitathmini mwenendo wa uchumi ulivyokuwa Mei. Kwa maana nyingine, ripoti ya mwezi wa kufunga mwaka wa fedha 2016/2017 haikutolewa pamoja na miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu wa fedha, 2017/18.
Baadhi ya wakosoaji wanatuhumu kuwa kutotolewa kwa taarifa hiyo kwa muda mrefu ni mwanzo wa uendeshaji uchumi kwa kificho baada ya Tanzania kujiondoa kwenye Mpango wa Uwazi Serikalini (OGP).
Kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook, akiituhumu Serikali kuwanyima wananchi taarifa kuhusu uchumi.
“Kwa kuchelewa huku, taarifa itakayotoka lazima itakuwa ya kupikwa,” amedai mbunge huyo wa Kigoma Mjini.
Kwa mujibu wa Sheria ya Benki Kuu ya mwaka 2006, BoT inalazimika kutoa taarifa za kila mwezi, robo mwaka na mwaka.
@habari na mwananchi

Zaidi ya watu 20 wauawa kwa wapigwa risasi Las Vegas Marekani

People fleeing from scene of country music festivalHaki miliki ya picha
Image captionWatu wengi wauawa kwa kupigwa risasi mjini Las Vegas Marekani
Zaidi ya watu 20 wameuawa na takriban 100 kujeruhiwa kwenye ufyatuaji wa risasi wakati wa tamasha huku Las Vegas. Marekani.
Mtu mwenye bunduki aliafyatua risasi kutoka ghoroga ya 32 kwenye hoteli ya Mandalay Bay, kwenda kwa tamasha lililokuwa likiendelea nje.
Eneo la mauaji
Image captionEneo la mauaji
Polisi wanasema mshukiwa ambaye alitajwa kuwa makaazi wa mji huo na ambaye hakutajwa jina ameuawa.
Mamia ya watu walikimbia eneo hilo na milio ya risasi ikasikika kwa muda kwenye video zilizochapishwa katika mitandao ya kijamii.
Ufyatuaji huo ulitokea mwendo wa saa 05:30 GMT na walioshuhudia walisema kuwa mamia ya risasi zilifyatuliwa.
Usafiri wa ndege ulisitishwa kutoka uwanja wa ndege wa McCarran mjini Las Vegas
People fleeing from scene of shootingHaki miliki ya picha
Image captionWatu wengi wapigwa risasi mjini Las Vegas Marekani
Police are seen crouching in front of vehicle outside hotelHaki miliki ya picha
Image captionPolisi wakiwa nje ya hoteli ya Mandalay@habari na bbc swahili

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...