Na IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 27 Mei, 2017 amemuapisha Bw. Tixon Tuyangine Nzunda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) - anayeshughulikia Elimu.

Viongozi wengine walioapishwa na Mhe.Rais Dkt. Magufuli ni Bwa. Rajab Omar Luhwavi ambaye anakuwa Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji,Bw. Bernard Mtandi Makali ameapishwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa na Bw. Clifford Katondo Tandari, kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro.
Pia Rais Magufuli amemuapisha Bw. Geoffrey Idelphonce Mwambe kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).
Rais Magufuli akimuapisha Ndugu Geoffrey Idelphonce Mwambe kuwa Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Ikulu jijini Dar es salaam Mei 27,2017
Viongozi wote walioapishwa wameahidi kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi wa hali ya juu katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Hafla ya kuapishwa viongozi hao imehudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Augustine Mahiga na viongozi mbalimbali wa Serikali.
No comments:
Post a Comment