DODOMA
Spika wa Bunge wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai amefunguka kuwa wabunge wanaodai kuwa
bunge ni dhaifu basi ni wazi watakuwa na mambo yanawasumbua ndio maana wanatoa
kauli za kudhihaki chombo hicho.
Mhe.
Ndugai amesema hayo leo mjini Dodoma baada ya kuwepo kwa baadhi ya
wabunge wanaotoa kauli zisizokuwa rasmi katika vikao vya
bunge bila kufikiria kwamba wanachokifanya hakina taswira nzuri kwa
wapiga kura wao pamoja na kwa serikali kwa ujumla.
"Yupo
mwenzetu alisimama hapa na kulalamika kuwa bunge hili ni dhaifu, kwa maoni
yangu hizi ni lugha za kuudhi kwa sababu wenzako wengi namna hii waliochaguliwa
na watu wakaletwa hapa halafu wewe unawaona kwa wingi wao ni dhaifu haipendezi.
Unajua sisi tunaokaa hapa mezani hatuchangii kama nyinyi, kazi yetu ni kuwapa
nafasi mseme, wakati mwingine zinatoka shutuma ambazo hatuna nafasi ya
kubishana au kulumbana lakini wakati mwingine ni vizuri kutumia fursa hizi
kusafisha baadhi ya mambo. Binadamu ni lazima uwe na staha ile ndogo tu
kuwaheshimu binadamu wenzako," alisema
Ndungai
Pamoja
na hayo, Ndugai ameendelea kwa kusema "Katika bunge letu
kinacholeta matatizo humu ndani ni tabia na lugha, tukirekebisha hayo mawili
tutaenda vizuri tu lakini najua kundi hili ni kubwa hatuwezi kuwa wote tupo
sawa, nitaendelea kulisemea lakini pale kwenye ulazima tutachukua hatua," alisisitiza
Ndugai.
Spika wa BUNGE Job Ndugai