HOFU
imezuka katika kijiji cha Katani kata ya Nkandasi wilayani Nkasi mkoani Rukwa
na kupelekea waombolezaji kutimua mbio na kuacha jeneza lenye mwili wa marehemu
baada ya mvua kubwa kuanza kunyesha na kubomoa nyumba za wakazi wa kijiji
hicho.
Mwenyekiti
wa serikali ya kitongoji cha Kaungo,Robert Kanoni amesema tukio hilo limetokea
wakati wakielekea kufanya maziko ya marehemu Dismas Kanoni aliyefari Juzi kwa
kuugua.
Amesema
ghafla mvua kubwa ilianza kunyesha ikiambatana na radi na upepo mkali hali
iliyosababisha baadhi ya waombolezaji kukimbia na kurejea majumbani kwao kutokana
na hofu iliyoibuka kufuatia tukio hilo.
Nyumba
zipatazo 10 zimeharibiwa sana zinatakiwa kujengwa upya huku nyumba nyingine
Saba zikiwa zimeezuliwa paa na wahanga kwa sasa wanategemea msaada wa majirani.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa kamati ya maafa ya wilaya hiyo Said Mtanda ambaye pia
ni mkuu wa wilaya ya Nkasi,amekiri kutokea kwa tukio hilo na kutoa wito
kwa wananchi kujenga makazi bora kwani miongoni mwa nyumba hizo zipo
ambazo zimeezekwa kwa nyasi.
Source:Gurian
No comments:
Post a Comment