Waziri Mkuu Kassim Majaliwa |
DAR ES SALAAM
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amemtaka Inspekta Jenerali wa Polisi,Simon Sirro
kuwakamata,Bw. Bahman wa kampuni ya NAS na Wakala wa Kampuni ya Wallmark Bw.Samwel
kwa kutaka kutoa bandarini magari makubwa aina ya semi tela 44 bila ya kulipa
kodi kwa kutumia jina la Waziri Mkuu.
Majaliwa
ametoa agizo hilo mara baada ya kufanya ziara ya ghafla bandarini baada ya
kupata taarifa za mfanyabiashara huyo aliyetaka kuutapeli uongozi wa TPA kutaka
kutoa magari hayo yaliyoingizwa nchini mwaka 2015 kutoka nchini Uturuki.
Aidha,Waziri
Mkuu ameitaka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kufanya kazi kwa
mujibu wa sheria na kutowasikiliza wafanyabiashara wanaotaka kukwepa kodi kwa
madai ya kupewa vibali vya msamaha wa kodi kutoka kwa viongozi wa juu
Serikalini.
Hatua
hiyo imekuja baada ya Bw.Bahman wa kampuni ya NAS kutaka kupata msamaha
wa kodi kwa kuidanganya TPA kwa madai kuwa wamewasiliana na Waziri Mkuu
na wasipotekeleza jambo hilo watapata matatizo.
Source:EATV
No comments:
Post a Comment