ZANZIBAR.
Kesi za udhalilishaji wanawake na
watoto katika mkoa wa Mjini Magharibi Unguja zimepungua kuanzia Januari hadi
Septemba 2017 ukilinganisha na mwaka jana.
Kesi hizo zilizokuwa zimeshika kasi
kisiwani Zanzibar zimepungua kutoka 633 kipindi kama hicho mwaka jana hadi
kufikia 404 mwaka huu.
Mratibu Msaidizi Dawati la Jinsia
Wanawake na Watoto mkoani humo, Kassim Fadhil amesema hayo jana katika
maadhimisho ya siku 16 za kupinga vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia
yaliyofanyika Madema mjini Unguja.
Amesema kasi ya kupungua vitendo
hivyo imekuja baada ya ushirikiano kati ya wananchi, taasisi za kiraia na Jeshi
la Polisi ambalo ni wahusika wakuu wa kupinga matendo hayo dhidi ya raia.
Mkurugenzi Msaidizi Dawati la Jinsia
Wanawake na Watoto Mjini Magharibi Unguja, Zahor Khamis amesema kwamba
wanadhamira kuweka vitengo maalumu vya usuluhisho na utoaji wa elimu ya kutosha
kwa baadhi ya wanandoa watakaobainika kuwa na matatizo ya udhalilishaji.
CHANZO: MWANANCHI.
No comments:
Post a Comment