Mkuu wa jeshi la polisi nchini (IGP) Simon Sirro |
PWANI.
Mkuu wa jeshi la polisi
nchini (IGP) Simon Sirro amewataka wazazi na walimu wilayani Kibiti na Rufiji,
kutoa taarifa kwenye vyombo vya dola juu ya kutoweka kwa wanafunzi zaidi ya
1,300 wakati wa matukio ya kiuhalifu yaliyotokea katika wilaya hizo.
Katika ziara yake ya kikazi wilayani Kibaha, mkoani
Pwani IGP amezungumza na wazazi, walimu pamoja na viongozi wa mashirika ya
umma,wazee maarufu, wastaafu mbalimbali na kamati ya ulinzi na usalama mkoani
humo.
IGP Sirro amewataka wazazi husika na walimu wa shule
za msingi na sekondari ambazo wanafunzi walikuwa ni watoro ama hawajaripoti
shule kwa miezi kadhaa kutoa taarifa kwani wapo baadhi ya watoto wanaotumika
kufundishwa uhalifu hata wakutumia silaha na watu wasiowema.
Kamanda Sirro ameeleza kuwa taarifa ya wanafunzi zaidi
ya 1,300 mkoani hapo kuwa ni watoro na hawajulikani walipo hivyo wazazi
washirikiane kusaidia jeshi la polisi kujua walipo.
Mkuu huyo wa jeshi la
polisi amewahakikishia wananchi mkoani Pwani kuwa silaha zote zilizochukuliwa
na wahalifu wa huko Kibiti na Mkuranga zimerudi zote mkononi mwa dola na
kusambaratisha mtandao wa kiuhalifu na wanaendelea kushirikiana na Msumbiji
kutokomeza uhalifu.
CHANZO: EATV.
No comments:
Post a Comment