kiongozi wa upinzani nchini kenya Raila Odinga |
NAIROBI.
Kiongozi wa Upinzani nchini Kenya NASA, Raila Odinga amesema anatarajia
kuapishwa kuwa Rais wa nchi hiyo Desemba 12, mwaka huu ambayo
itakuwa siku ya uhuru wa Kenya.
Odinga ametoa kauli hiyo ikiwa katika uwanja wa
Jacaranda saa chache baada ya Rais Kenyatta kuapishwa kuwa Rais wa nchi hiyo
katika uwanja wa Kasarani.
Hata hivyo, wakati Odinga akisema hayo, Rais Kenyatta
mara baada ya kuapa amewaambia wananchi wa Kenya kuwa hakutakuwa na
shughuli zingine za uchaguzi na yeye ndiye Rais mteule wa Kenya.
Hata hivyo, Polisi nchini Kenya walivamia uwanja
uliopangwa kufanyika mkutano na maombolezo ya wananchi waliofariki wakati wa
vurugu za uchaguzi wa marudio uliofanyika Oktoba 26, mwaka huu.
Rais Uhuru Kenyatta ameapishwa jana kuwa Rais wa Kenya ili kuwatumikia
wakenya katika muhula wa pili wa uongozi.
CHANZO: EATV.
No comments:
Post a Comment