Mkuu wa wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi Swalehe Muhando
TANGANYIKA
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando
amesema kuwa watahakikisha kunakuwepo na
ukaguzi wa vyombo vya usafirishaji katika mwambao wa ziwa Tanganyika ili kuzuia
usafirishaji wa mazao kwenda nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Akizungumza na Mpanda Radio Mapema leo
amesema kuwa mazao ya chakula hayatasafirishwa mpaka kuwepo na kibali maalumu,
huku akisema watashirikiana na mikoa jirani ili kuhakikisha marufuku hiyo
inatekelezwa.
Mhando amesema kuwa kwa mfanyabiashara yeyote
atakaye kamatwa akisafirisha mazao kwenda nje ya nchi hatua za kisheria zitachukuliwa kama vile kutaifishwa kwa mazao
hayo na gari lililobeba mazao hayo.
Mapema wiki hii, waziri mkuu Kasim Majaliwa
katika sherehe za Idd el fitri zilizofanyika Kilimanjaro alipiga marufuku
usafirishaji wa mazao ya chakula nje ya nchi, kauli ambayo ameisisitiza jana
bungeni mjini Dodoma
No comments:
Post a Comment