Mkuu wa Oparesheni maalumu ya jeshi
la polisi, Naibu Kamishna, Liberatus Sabasi
Jeshi la polisi limefanikiwa kuwaua
kwa risasi watu wanne wanaosaidikiwa kuwa miongoni mwa wahalifu wanaoendesha
mauaji katika wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji mkoani Pwani.
Mkuu wa Oparesheni maalumu ya jeshi
la polisi, Naibu Kamishna, Liberatus Sabas alisema tukio hilo lilitokea siku ya
Alhamisi Juni 29 majira ya saa tatu usiku kwenye barabara ya vumbi itokayo
Pagae kuelekea Nyambunda, ambapo askari polisi wakiwa katika doria walikutana
na kikundi cha watu sita, watu hao baada ya kuona gari la polisi walikimbilia
vichakani na kuanza kuwarushia risasi Polisi.
Sabas anadai katika mapambano hayo
yaliyodumu kwa nusu saa, polisi walifanikiwa kuwajeruhi kwa risasi watuhumiwa
nne ambao baadaye walifariki dunia wakiwa wanapelekwa hospitali kwa ajili ya
kupatiwa matibabu.
"Katika
tukio hilo tumefanikiwa kupata silaha mbili aina ya SMG na magazine mbili
pamoja na risasi 17 zilizokuwa zinatumiwa na wahalifu hao na hii ni dalili kuwa
tunaendelea vizuri na oparesheni yetu ambayo inashirikisha vyombo vingine vya
ulinzi na usalama katika wilaya hizi tatu za Mkuranga, Kibiti, na
Rufiji":- alisema
Naibu Kamishna, Liberatus Sabas
Mbali na hilo Naibu Kamishna,
Liberatus Sabas amewataka wahalifu wengine kuacha mara moja vitendo hivyo na
kusema vyombo vya usalama vipo kazini kuhakikisha usalama wa eneo la Pwani
unakuwepo siku zote.
Mpaka sasa ni zaidi ya watu 30
wamepoteza maisha kwa kuuwawa wakiwemo askari polisi pamoja na viongozi
mbalimbali hususani viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
No comments:
Post a Comment