Tuesday, 1 August 2017

Wapigapicha marufuku ndani ya vituo vya kura

TUME Huru ya Uchaguzi nchini Kenya (IEBC) imepiga marufuku wapigapicha ndani ya vituo vya kupigia kura, pia haitaruhusiwa kujipiga picha wakati wakipiga kura.

 Mwenyekiti wa tume hiyo, Wafula Chebukati, pia amepiga marufuku, wapigakura kupiga picha karatasi za kupigia kura wakionesha wamemchagua nani.

 Ni waandishi wa habari pekee wenye vibali ndio watakaoruhusisiwa kupiga picha na kuandika habari za uchaguzi ifikapo siku ya uchaguzi Agosti 8, mwaka huu.

 Hata hivyo, waandishi na wapigapicha hao, wataruhusiwa tu kuandika na kupiga picha mwenendo mzima wa uchaguzi na si vinginevyo.
 “Upigaji kura ni kitendo cha siri.Ni makosa kuonesha kila mtu au kutuma kwenye mitandao ya kijamii umempigia kura nani,” alisema Chebukati.

 Mwenyekiti huyo alisisitiza kuwa katazo hilo limelenga kulinda haki ya mpiga kura kutunza siri yake kwa mujibu wa Sheria na kuzuia kushawishi wengine kumpigia kura kiongozi asiyemtaka.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...