Mbunge wa Kilombero mkoani Morogoro, Peter Lijualikali
ameshikiliwa na kuhojiwa na polisi wilayani Malinyi kwa saa nne.
Pamoja naye, viongozi wengine watatu wa Chadema
walishikiliwa jana wakidaiwa kufanya mkusanyiko bila kuwa na kibali
cha polisi.
Akizungumza leo baada ya kuachiwa mbunge huyo amesema
aliamriwa na polisi kusimama alipokuwa akitoka kwenye kikao cha ndani cha
viongozi na baadhi ya wanachama wa Chadema katika Kijiji cha Makerere wilayani
Malinyi.
Mbunge huyo amesemabaada ya kumpigia simu Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei amejibiwa yupo likizo.
Wengine waliokamatwa pamoja na mbunge huyo ni Mwenyekiti wa
Chadema Malinyi, Emmanuel Lukindo; Katibu wake, Sadi Lyampawe na Katibu Mwenezi
wa wilaya, Lucas Lyambalimu ambao wote wameachiwa kwa dhamana
No comments:
Post a Comment