Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan |
DAR ES
SALAAM
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufungua mkutano wa mwaka
wa Chama cha Majaji na Mahakimu wa nchi za Jumuiya ya Madola unaofanyika nchini
kwa mara ya kwanza kuanzia Septemba 24 hadi 28 mwaka huu.
Hilo limethibitishwa leo na Jaji
Mkuu Profesa Ibrahimu Juma kwenye ukumbi wa Mahakama ya rufaa jijini Dar es
salaam.
Jaji Ibrahimu amesema Makamu wa Rais
atafungua mkutano huo ambao unatarajiwa kuhudhuriwa na washiriki wapatao 354
kutoka nchi mbalimbali za Jumuiya ya Madola.
Jaji Mkuu amesema katika mkutano huo
Tanzania itawakilishwa na wajumbe 50 ambao ni Majaji na mawakili kutoka
Tanzania bara na visiwani.
Ujumbe mwingine mzito wa watu 13
ambao ni Marais na Majaji kutoka Austaria, Zambia, Afrika Mashariki na
Pakistani utakuwepo kwenye mkutano huo.
Aidha Jaji amebainisha kuwa Rais wa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Mohamed Ali Shein atafunga mkutano huo
mnamo Septemba 28 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment