MPANDA.
Baadhi ya watahiniwa wa
mtihani wa kidato cha nne katika shule mbalimbali manispaa ya Mpanda Mkoani
hapa wameeleza matumaini ya kufaulu mtihani wao ulionza leo nchi nzima.
Wakizungumza na Mpanda
Redio kwa nyakati tofauti wanafunzi hao wakiwemo wa shule ya sekondari mwangaza
na kashaulili wamesema maandalizi yao katika mtihani huo yako vizuri huku
wakiwaomba wenzao kuondoa hofu ya mtihani.
Kwa upande wake Mkuu wa
shule ya sekondari Mwangaza Mwl. Simoni Lubange amewataka wanafunzi wake
kujiamini na kumtanguliza mungu katika ujibuji wa mitihani yao kwa alichokisema
hakuna kitu kigeni watakachokutana nacho.
Jumla ya watahiniwa
385, 938 wa kidato cha nne nchini wameanza mtihani leo huku baraza la mitihani
likitoa onyo kwa na tahadhari kwa wamiliki wa shule watakaofanya udanganyifu.
No comments:
Post a Comment