MPANDA.
IDARA ya uvuvi Mkoani Katavi
imezindua mafunzo ya siku kumi ya uvuvi,uchakataji na usindikaji wa mazao ya
samaki.
Afisa
Uvuvi Mkoani Katavi Kayumba Torokoko amesema lengo la kuendesha semina
hiyo inayofanyika Tarafa ya Karema Wilayani Tanganyika inalenga kuelimisha
wachakataji wengi kujua namna ya
kuhifadhi samaki kwa njia ya kisasa zaidi.
Amesema mafunzo hayo yatakayodumu kwa
siku kumi yatapelekea vikundi vingi vya kuchakata samaki kuwa katika ubora
mzuri ili kupata soko zuri.
Kwa upande wake Afisa maendeleo ya
jamii Tarafa ya Karema Mary Patric Kawogo amesema mafunzo hayo yataongeza uwezo
wa wachakataji wa samaki ili ili kuendesha shghuli yenye tija.
Nao baadhi ya washiriki wa semina
hiyo wamesema kupitia mafunzo hayo watajua namna ya kuinua kipato na kuimarika kiuchumi.
@habari na Rehema Msigwa
No comments:
Post a Comment