KATAVI.
Wamiliki na madereva wa vyombo vya moto
Mkoani Katavi wametakiwa kuhakikisha vyombo vyao vya usafiri vinafanyiwa
ukaguzi.
Agizo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa
kamati ya usalama Barabarani Mkoani Katavi Nassoro Alphi wakati akizungumza na
Mpanda Redio kwa njia ya simu na kusema kuwa zoezi hilo linafanyika nchi nzima
na litadumu kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Amesema kuwa kwa mkoa wa katavi wameanza
na magari ya abiria pamoja na Malori na ofisi ya Mkuu wa kitengo cha usalama
barabarani imetoa wiki tatu ya ukaguzi wa hiari nje ya hapo zoezi la kukamata
litaanza.
TEMBO MZEE Amesema lengo la kufanya ukaguzi huo ni kuhakikisha magari yote yanakuwa katika hali ya ubora na ambaye gari lake halitakaguliwa hata patiwa stika.
HABARI NA MDAKI HUSEIN
No comments:
Post a Comment