Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya Mpanda Michael Nzyungu |
MPANDA.
Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya
Mpanda Michael Nzyungu ameagiza kuajiriwa kwa baadhi ya maafisa kata wa muda
katika baadhi ya Kata.
Amesema hayo katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika jana katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda alipokuwa akijibu baadhi ya maswali yaliyo ulizwa na Waheshimiwa madiwani kuhusu tatizo hilo.
Katika hatua nyingine amezitaja baadhi
ya sababu zilizopelekea upungufu wa watendaji hao kuwa ni baadhi yao kukumbwa
na sakata la watumishi wenye vyeti feki.
Baraza la Madiwani linaendelea leo
ambapo Madiwani watawasilisha mapendekezo mbali mbali ya utekelezwaji wa bajeti
katika kata zao.
HABARI NA ALINANUSWE EDWARD
No comments:
Post a Comment