DAR ES SALAAM
UONGOZI wa Mamlaka ya Usimamizi wa
Bandari Tanzania (TPA), umetekeleza agizo la Rais John Magufuli la kufungua ofisi zake nchini Rwanda kwa lengo la kuwaondolea usumbufu wafanyabiashara wa nchi
hiyo.
Haya yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa
TPA, Deusdedit Kakoko hivi karibuni alipokutana na Balozi wa Rwanda nchini
Tanzania, Eugene Kayihura aliyeitembelea mamlaka hiyo.
TPA imeshakamilisha taratibu zote na
tayari ina ofisi na mtumishi wake nchini humo, hivyo kinachosubiriwa kwa sasa
ni ufunguzi rasmi wa ofisi hiyo jijini Kigali.
Hatua hiyo imepongezwa na Balozi
Kayihura, akisema anaushukuru uongozi wa TPA na Serikali ya Tanzania kwa
kuwajali watu wa Rwanda.
Balozi Kayihura ameeleza kuwa biashara kati ya Tanzania na Rwanda
imekuwa ikiongezeka kwa kasi katika siku za hivi karibuni baada ya TPA
kuimarisha huduma zake.
Source TBC 1
Editor
REBECCA KIJA
No comments:
Post a Comment