Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Katavi Damasi Nyanda |
MPANDA
Baadhi ya Wananchi kata ya Misukumilo Manispaa ya Mpanda wamedai kuingiwa na hofu kufuatia kukithiri kwa matukio ya kiharifu katika eneo la linalofahamika kwa jina la Migazini.
Wakizungumza na mpanda redio fm wakazi hao wamesema kuwa vitendo vya kiharifu katika eneo la migazini vimekithiri hivyo kuliomba jeshi la polisi kushughulikia tatizo hilo.
Afisa mtendaji wa kata hiyo Pasca Mbete amekili kuwepo kwa vitendo hivyo na kuahidi kuimarisha ulinzi na usalama ili kuondoa adha hiyo.
Kwa upande wa Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Katavi Damasi Nyanda amewataka wananchi kutoa ushirikiano ili kuwabaini waharifu hao.
SOURCE: REHEMA
Msigwa
No comments:
Post a Comment