Wednesday, 6 December 2017

Serikali imezindua mwongozo wa huduma za maji na usafi wa mazingira katika vituo vya tiba ikiwemo zahanati

Mkurugenzi wa Sekta Ofisi ya Rais Tamisemi, Dk Andrew Komba 


DODOMA

Serikali imezindua mwongozo wa huduma za maji na usafi wa mazingira katika vituo vya tiba ikiwemo zahanati, vituo vya afya na hospitali.

Mkurugenzi wa Sekta Ofisi ya Rais Tamisemi, Dk Andrew Komba amesema uzinduzi wa mwongozo huo ni katika kueleka awamu ya pili ya kampeni hiyo itakayozinduliwa rasmi na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ifikapo Desemba 7 mjini Dodoma.

Naye Mratibu wa Kampeni ya Kitaifa ya Usafi ya Mazingira, Anyitike Mwakitalima amesema  kwamba kisababishi kimojawapo ilikuwa ni ukosefu wa mwongozo wa taifa ambao wadau na serikali wangeutumia kusimamia usafi wa mazingira.

 Aidha amesema malengo ya kitaifa ifikapo June 2021 ni kuhakikisha hakuna kaya isiyo na choo.

Haya yote yanafanyika ikiwa ni katika kuelekea uzinduzi wa awamu ya pili ya  kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira.



SOURCE:Eatv

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...