DAR
ES SALAAM.
Wananchi
wametakiwa kutoa taarifa wanapoona upatikanaji wa dawa katika vituo vya afya si
wa kuridhisha.
Kaimu
mkurugenzi wa fedha na mipango wa MSD Sako Mwakalobo, amesema hayo wakati wa uzinduzi wa mpango
mkakati wa kati uliopitiwa upya ambao utakamilika ifikapo 2020.
Mwakalobo
amesema Wizara ya Afya imeweka mifumo rahisi ya kutoa taarifa ya ukosefu wa
dawa na kuna nafasi ya malalamiko kupelekwa kwa mganga wa eneo husika au
kupiga kwa mfamasia mkuu wa Serikali.
Mwakalobo
amesema ununuzi na usambazaji wa dawa unafanyika kwa asilimia 80 na hadi
kufikia Machi mwakani huduma itafikia asilimia 100.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk Mpoki Ulisubisya ameitaka MSD kuongeza kasi ili
kwendana na wakati uliopo.
SOURCE:MWANANCHI
No comments:
Post a Comment