Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi |
DAR ES SAALAM
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, amewataka
wamiliki wa nyumba nchini kuwapa fursa wapangaji kulipa kodi ya mwezi
mmoja mmoja badala ya miezi sita au mwaka.
Waziri Lukuvi ameyasema hayo wakati akifungua jengo la ofisi ya makao makuu
ya shirika la nyumba nchini (NHC).
Lukuvi amesisitiza kuwa wamiliki
wa nyumba kuanzia sasa wanatakiwa kulipwa kila mwezi, ili iwape fursa wapangaji
kuwa na maisha yanayowezekana kuishi maeneo ya mjini.
Hivi karibuni kumekuwepo na
mjadala kuhusu namna ya kulipa kodi baada ya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mh. Angelina Mabula kuweka wazi kuwa wizara hiyo iko mbioni
kuja na sheria itakayomwezesha mpangaji kulipa kodi kwa mwezi mmoja mmoja.
SOURCE: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment