Wednesday, 6 December 2017

Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa wamesema watawaondoa zaidi ya wahamiaji 15,000 waliokwama nchini Libya ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.


ADIS ABABA

Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa wamesema watawaondoa zaidi ya wahamiaji 15,000 waliokwama nchini Libya ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

 Tangazo hilo linakuja baada ya kufanyika mkutano wa kilele kati ya Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa wiki iliyopita nchini Cote d'Ivoire ambapo viongozi wa Afrika na Ulaya wamekubaliana kuwaondoa kiasi ya wahamiaji 4,000 waliokwama nchini Libya.

Wahamiaji kati ya 400,000 na 700,000 wengi wao kutoka mataifa ya kusini mwa jangwa la Sahara inaripotiwa wanaishi katika makambi kadhaa nchini Libya.

  Umoja wa Mataifa ukikadiria kuwa kuna zaidi ya wahamiaji milioni tano

 SOURCE:BBC

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...