Wednesday, 6 December 2017

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limeshutumu ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi ya jamii ya Warohingya nchini Myanmar.


JOHANNESBURG

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limeshutumu ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi ya jamii ya Warohingya nchini Myanmar.

 Kamishina mkuu wa haki za binadamu Zeid Raad al-Hussein amesema  mjini Geneva kuwa licha ya makubaliano kati ya Myanmar na Bangladesh, Waislamu wachache wa jamii ya Rohingya wamekuwa wakiendelea kukimbia makazi yao kwa ajili ya kutafuta usalama.

 Shahriar Alam, waziri mdogo wa mambo ya nje amesema idadi inaweza kukaribia milioni moja.

 Baraza hilo la Umoja wa Mataifa pia limetoa mwito kwa serikali kuhakikisha haki inatendeka kwa waathirika na pia wachunguzi dhidi ya tuhuma hizo na wafanyakazi wa mashirika ya misaada waruhusiwe kuingia kirahisi katika jimbo la Rakhine.


 SOURCE:Bbc swahil

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...