WASHINGTON DC
Ikulu ya Marekani imesema inapanga kuanzisha upya juhudi za
kufikiwa makubaliano ya amani kati ya Israel na Palestina licha ya uamuzi wa
Rais Donald Trump kuitambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.
Maafisa wa utawala wa Marekani wamesema juhudi hizo huenda
zikafufuliwa wiki ijayo kukiwa na matumaini kuwa ghadhabu dhidi ya hatua
aliyoichukua Trump itakuwa imepungua.
Rais Mahamoud Abbas wa Palestina alitangaza mapema wiki hii
kuwa Wapalestina hawatakubali Marekani kuwa na jukumu lolote katika mchakato wa
kutafuta amani katika mzozo wa Mashariki ya Kati kwa sababu Marekani
inaipendelea Israel.
Kufuatia hatua hiyo,viongozi wa Palestina walisema hawatakutana
na Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence anayetarajiwa kuwasili mjini Jerusalem
Jumatano ijayo kwa ziara Mashariki ya Kati.
Ikulu ya Marekani imesema inatumai ziara ya Pence itakuwa
sehemu ya kile ilichokitaja kama kufungwa kwa ukurasa mmoja na kufunguliwa
mwingine wakiendelea kuangazia kufikiwa kwa amani Mashariki ya Kati.
Chanzo:Dw swahil
No comments:
Post a Comment