Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd |
ZANZIBAR
Makamu
wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd amesema ushauri wa wajumbe wa
Baraza la Wawakilishi kutaka kuongezwa muda wa urais kutoka miaka mitano mpaka
miaka saba ni suala zuri na linazungumzika bila matatizo.
Balozi
Idd amebainisha hatua hiyo wakati akifunga mkutano wa nane wa Baraza la Tisa la
Wawakilishi lililochukua muda wa wiki moja Mjini Zanzibar.
Awali
baadhi ya wajumbe wa baraza hilo wakichangia Muswada wa Sheria ya Marekebisho
ya Tume ya Uchaguzi ya mwaka 1984 na kuweka sheria ya mwaka 2017 wamesema ili
Zanzibar iepukane na matumizi hasa kipindi cha uchaguzi hakuna budi kuongezwa
kwa muda wa utumishi wa urais.
Hata
hivyo,Balozi Iddi akifunga mkutano huo amesema Serikali imedhamiria kukabiliana
na changamoto zinazowakabili wananchi wake ili kuona nao wanaishi katika hali
ya matumiani.
No comments:
Post a Comment