Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Simon |
RUKWA
Mkuu
wa jeshi la polisi nchini IGP Simon amewaomba viongozi wa dini mkoani Rukwa,Kuongeza
bidii katika kuhubiri amani ili mauaji yanayotokayo na imani za kishirikina na wivu
wa kimapenzi yapungue mkoani humo.
IGP
Sirro ametoa kauli hiyo wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka
kujua mikakati ya jeshi hilo katika kukabiliana na mauaji mkoani humo.
Amesema
jeshi la polisi linajitahidi kukabiliana na mauaji yote yanayotokea nchini
lakini katika Mkoa wa Rukwa takwimu zinaonesha kuwa mauaji yanayotokana na
ushirikina pamoja na wivu wa mapenzi yanaongoza mkoani humo.
Wakati
huo huo IGP Sirro ameahidi kuwa Jeshi hilo kupitia bajeti zake litajenga kituo
kipya cha polisi cha Sumbawanga mjini ambacho ni chakavu kwa sasa huku akiahidi
pia kuupatia mkoa wa Rukwa gari moja jipya aina ya Lori litakalosaidia kutumika
katika matumizi mbalimbali ya polisi mkoani humo.
Kwa
upande wake Mwenyekiti kamati ya wa ulinzi na usalama mkoani Rukwa Joachim
Wangabo ambaye pia ni mkuu wa mkoa huo amemwambia IGP kuwa atajitahidi
kuwashirikisha wafanyabiashara mkoani humo ili wajenge nyumba za kuishi polisi
kwa kuwa hawawezi kusubiri mpaka serikali ifanye kazi hiyo.
No comments:
Post a Comment