Friday, 1 December 2017

Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Stephen Kagaigai amesema amemwandikia barua kaka wa mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu akimtaka alieleze bunge ni stahiki zipi ambazo ndugu yao anastahili apewe na chombo hicho.

Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Stephen Kagaigai 

DODOMA 
Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Stephen Kagaigai amesema amemwandikia barua kaka wa mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu akimtaka alieleze bunge ni stahiki zipi ambazo ndugu yao anastahili apewe na chombo hicho.
Kauli hiyo inayoweza kuibua malumbano mapya katika matibabu ya mwanasheria huyo mkuu wa Chadema, imetolewa siku mbili baada ya Lissu kuhoji sababu za Bunge kutojihusisha na matibabu yake tofauti na sheria zinavyotaka.
Lissu yuko Hospitali ya Nairobi nchini Kenya ambako anatibiwa tangu Septemba 7 aliposhambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana akiwa ndani ya gari nje ya makazi yake mjini Dodoma.

Kauli ya Lissu ilikuwa ni mwendelezo wa kilio kilichotolewa awali na ndugu yake,Alute Mughwai Lissu ambaye alisema alishaiandikia ofisi ya Bunge kutaka ilipie gharama za matibabu ya mbunge huyo.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...