MOROGORO
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani
Morogoro imewanyima dhamana Wabunge Peter Lijualikali,Suzan Kiwanga na wafuasi
wengine 34 wa Chadema wakiwemo madiwani na kuwarudisha mahabusu hadi Disemba 04
mwaka huu.
Wabunge hao walikamatwa wiki hii kwa
tuhuma za kufanya vurugu katika uchaguzi wa madiwani ikiwa ni pamoja na kuchoma
shule na rasilimali nyingine za umma.
Polisi mkoani Morogoro iliwatia
mbaroni watuhumiwa 41 kwa madai ya kufanya fujo na kuchoma moto majengo
ya shule baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Sofi
Kamanda wa Polisi Ulrch Matei amesema
Viongozi hao walikuwa wakiwachochea wafuasi wa chama hicho kuchoma moto
nyumba ya walimu wa shule ya kata ya Sofi na ofisi ya Afisa mtendaji kata
kwa kutumia petrol ambapo baadaye walidhamiria kuchoma zahanati lakini askari
wakawakamata.
Mbunge Lijualikali yeye
alijisalimisha baada ya kupata taarifa kwamba anatafutwa
Source:Mwananchi
No comments:
Post a Comment