Friday, 19 January 2018

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeonesha hofu kwa viongozi wakuu wa kitaifa wanaofanya safari kuelekea Makao Makuu ya nchi Dodoma, kudhurika kutokana na maji ya mvua kufunika barabara mara kwa mara katika eneo la Kibaigwa.

DAR ES SALAAM.

Kutokana na kutanda kwa hofu hiyo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amekubali ombi la wajumbe wa Kamati hiyo la kuambatana nao ili kufika katika eneo kubaini kiini cha hali hiyo.

 Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati  ya Bunge, Profesa Norman Sigala wakati kamati hiyo ilipokutana na Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB) katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.

Aidha ameongeza kusema mbali ya barabara hiyo ya Dodoma- Morogoro, ambayo hivi karibuni ikisababisha magari yanayokwenda na kutoka Mikoa ya Kanda ya Kati na nchi jirani kushindwa kupita katika eneo hilo kwa saa nane, Kamati hiyo imeagiza pia barabara ya Dodoma- Iringa katika eneo la Fufu kutazamwa.

Chanzo:Mwanachi

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...