Friday, 19 January 2018

Uagizaji wa dawa nje wagharimu Sh224 bilioni.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu 


DAR ES SALAAM

Serikali imesema kila mwaka inapoteza mapato ya dola 100 milioni (Sh224 bilioni kwa kuagiza dawa nje ya nchi.

Akizungumza katika uzinduzi wa toleo la tano la mwongozo wa matibabu nchini na orodha ya taifa ya dawa muhimu  Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema Serikali itaboresha upatikanaji wa dawa kwa kuimarisha sekta ya viwanda.

Ummy ameeleza kuwa kuboreshwa kwa sekta hiyo kutapunguza matumizi ya fedha za kigeni kuagiza dawa kutoka nje, badala yake kujikita katika kuimarisha uzalishaji wa dawa kwenye viwanda vya ndani.

Aidha amefafanua kuwa  katika kudhibiti kuenea kwa usugu wa vimelea vya magonjwa ya kuambukiza, mwongozo umefuata maelekezo yaliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) ambayo dawa aina ya antibiotiki zitatakiwa kutumika kwa umakini mkubwa.


Source Mwananchi

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...