Friday, 19 January 2018

Ripoti ya Shirika la kutetea haki za binaadamu la Human Right Watch ya mwaka 2018 imeangazia haki za binaadamu namna zilivyokiukwa katika mataifa kadhaa barani Afrika.


WASHINGTON

Ripoti ya Shirika la kutetea haki za binaadamu la Human Right Watch ya mwaka 2018 imeangazia haki za binaadamu namna zilivyokiukwa katika mataifa kadhaa barani Afrika.

 Ikianza na Tanzania, ripoti hiyo inasema baada ya kuingia serikali awamu ya tano ilidhamiria kuondoa tatizo la rushwa serikalini na kuongeza uwajibikaji kwa manufaa ya wananchi wa kawaida, lakini badala yake uhuru wa kukosoa umekandamizwa ikiwemo kufungwa kwa vyombo vya habari.

 Aidha imeeleza kuwa watetezi wa haki za binadamu, wanaharakati wa asasi za kiraia na maafisa waandamizi wa Umoja wa Mataifa wamekumbana na aina mbalimbali za vitisho na kuwekwa vizuizini bila sababu za msingi kunakofanywa na mamlaka za serikali.

 Nchini Kenya nako Shirika hilo limebaini kuwa mauaji yaliyofanywa na polisi katika mitaa ya mabanda hayakuchunguzwa hadi  leo.

Aidha katika kipindi cha kabla na baada ya uchaguzi shirika hilo limesema polisi na vikosi vingine vya usalama vimetumia nguvu kupita kiasi kuwakabili waandamanaji hasa katika ngome za upinzani.


Chanzo: Dw swahili

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...