Tuesday, 9 January 2018

Serikali imeviagiza vyombo vya usalama na kamati za Afya za vijiji kuimarisha mifumo ya udhibiti wa upotevu wa Dawa nchini.

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile


KIGOMA

Serikali imeviagiza vyombo vya usalama na kamati za Afya za vijiji kuimarisha mifumo ya udhibiti wa upotevu wa Dawa nchini, ili kuondoa ubadhilifu unaofanywa na baadhi ya watumishi wasio waaminifu.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile katika ziara yake  Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma ya kukagua utoaji huduma za Afya na kufuatilia utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya jamii .

Katika kupunguza vifo vya kina mama na watoto Dkt. Faustine amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imewekeza kiasi cha shilingi Milioni 400 katika Halmashauri 175, kikiwemo kituo cha Afya cha Uvinza.

 Nae Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Bi Mwanamvua Mlindoko ameeleza faida ya mradi wa ujenzi wa madarasa ikiwemo ongezeko la ufaulu kutoka wanafunzi 4115  mwaka 2017 huku waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza ni wanafunzi 1641 ambao ni sawa na asilimia 36.


Chanzo:Mwananchi

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...