TANGANYIKA
Wanufaika wa mfuko wa
kunusulu kaya Masikini Tasaf katika Kata ya Kabungu wilaya ya Tanganyika Mkoa
wa Katavi wameishukuru Serikali kwa kuanzisha mpango wa kuwapatia fedha za
kujikimu katika kaya zao.
Miongoni mwa wanufaika
wameuelezea mradi huo kuwasaidia kuleta
mageuzi katika kaya ikiwemo Ufugaji pamoja na ujenzi.
Pamoja na hayo wanaitaka
serikali kuangalia uwezekano wa kuongeza kiasi cha fedha kwaajiri ya mgao wa
kila kaya husika ili kuendana na maisha ya sasa.
Mkuu wa idara ya
maendeleo ya Jamii manispaa ya Mpanda bwana Kasala Bulemo amesema lengo la mradi huo ni kusaidia
kaya masikini kielimu, afya ikiwemo
uibuaji wa miradi midogo midogo katika kaya zao.
Zaidi ya wanufaika 145
wamepokea fedha kutoka mfuko wa kunusulu kaya masikini Tassaf katika kata ya
Kabungu wilayani Tanganyika.
No comments:
Post a Comment