Thursday, 1 February 2018

Mahakama Kuu Kenya yabatilisha ufungaji wa vituo vya habari.



KTN news presenter on airHaki miliki ya pichaKTN
Image captionVituo vya habari vilifungiwa lakini wakaendela kurusha matangazo kupitia mtandao
Mahakama Kuu nchini Kenya imeamuru kuwashwa kwa vituo vya habari vitatu binfasi na serikali na kuiagiza serikali kutoingilia utendaji kazi wa vituo hivyo hadi kesi hiyo itakaposikilizwa kikamilifu.
Siku ya Jumanne matangazo ya vituo vya KTN, NTVna Citizen TV yalizimwa ghafla na serikali baada ya mamlaka ya mawasiliano nchini Kenya kuzima mitambo yao kuepusha vituo hivyo kurusha moja kwa moja mkutano wa kuapishwa kwa kiongozi wa upinzani Raila Odinga kama Rais wa watu wa Kenya.
Bado haijulikani kama serikali wataifuatilia agizo hilo.
Sherehe ya kuapishwa kwa Raila ilichukuliwa na wengi kama mzaha lakini serikali imeshikilia kuwa kitendo hicho kilikuwa kinakiuka sheria za nchi hiyo na kwamba ni kosa la uhaini hivyo ilijaribu kuhakikisha taarifa hiyo haitawafikia Wakenya wengi ambao wangelifuatilia tukio hilo kupitia matangazo ya luninga
Okiya Omtata, muwasilishaji mashtaka na mwanaharakati amesema anataka agizo la serikali litangazwe kuwa kinyume na katiba na vituo hivyo vifidiwe.
The symbolic presidential oath of opposition leader Raila Odinga in Nairobi, Kenya, on 30 January 2018Haki miliki ya picha
Image captionRaila Odinga akila kiapo cha kuwa rais wa wananchi wa Kenya
Wakenya wengi wamekosa matangazo ya runinga kwa siku tatu sasa. Vituo hivyo vilivyoathirika vimedai kupata hasara ya mamilioni ya dola za kimarekani.
Vituo hivyo vya binafsi vinategemea fedha za matangazo ya biashara na hawakuweza kupata fedha hizo kwa siku zote walizokuwa wamefungiwa.
Bw Omtata ametaka serikali ilipie hasara za Citizen TV, KTN na NTV
Kuibuka kwa mitandao ya jamii kumeathiri vyanzo vya mapato vya vituo vingi vya habari na kulazimika kuwafuta kazi mamia ya wafanyakazi wao ndani ya mwaka mmoja uliopita.
Serikali ya Kenya ilitaka vituo hivyo vifungwe hadi polisi wamalize uchunguzi dhidi ya wanasiasa na waandishi walioshiriki katika sherehe ya kuapishwa kwa Bw. Odinga siku ya Jumanne.
Chanzo:Bbc swahili
#Changia Damu Okoa Taifa

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...