DAR ES SALAAM
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), limefuta
matokeo ya watahiniwa 265 waliobainika kufanya udanganyifu katika mtihani wa
kidato cha nne (CSEE) uliofanyika Oktoba, mwaka jana.
Baraza hilo limebainisha aina za udanganyifu
zilizofanywa na watahaniwa hao wakiwemo 136 wa kujitegemea na 129 wa shule kuwa
ni pamoja na kuingia kwenye chumba cha mtihani na vitu visivyotakiwa, kufanyiwa
mtihani na watu wengine, kubadilishana namba na karatasi za majibu na miandiko
tofauti.
Hayo yamebainishwa na
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dk Charles Msonde,
wakati akizungumza na vyombo vya habari Dar es Salaam kuhusu matokeo ya mtihani wa kidato
cha nne kwa watahiniwa waliofanya mtihani huo mwaka jana.
Aina nyingine ya udanganyifu ni watahiniwa kuwa na
mfanano wa majibu ya kukosa usio wa kawaida ambapo inasadikiwa walipatiwa
majibu na mwalimu wao ambaye hata hivyo naye hakuwa analifahamu jibu.
Chanzo:Habari Leo
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment