DODOMA
Vikao vya kamati za Bunge
vimeanza huku miongoni mwa miswada itakayojadiliwa ikiwa ni ule utakaoongeza
umri wa kustaafu kwa lazima kutoka miaka 60 hadi 65 kwa maprofesa, wahadhiri
waandamizi na madaktari bingwa wa magonjwa ya binadamu wa umma.
Marekebisho hayo yapo katika
Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba Tano wa Mwaka 2017 ambao
utazihusisha sheria tano ikiwamo ya Utumishi wa Umma sura namba 298 ambapo
kifungu kipya cha 25A kitaongezwa.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Katiba na Sheria inayoongozwa na Mohamed Mchengerwa ndio itakayojadili muswada
huo ambao utahusisha pia sheria nyingine tano.
Kwa mujibu wa Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, George Masaju lengo la kuongezwa kwa kifungu hicho ni kuweka kwenye
masharti ya umri wa kustaafu kwa watumishi wa umma ambayo hayapo kwenye sheria
ya sasa.
Chanzo: Mwananchi
No comments:
Post a Comment