Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa umma nchini wasijihusishe na
vitendo vya wizi, ufisadi kwani Serikali haitosubiri kuwaundia tume za
kuwachunguza bali itawashughulikia hapo hapo.
Majaliwa amesema hayo akiwa mkoani Mara Wilayani
Musoma na kudai kuwa Serikali haiko tayari kuwavumilia watumishi wanaojihusisha
na wizi, ubadhilifu, rushwa na uzembe, hivyo ni vema viongozi waliopewa dhamana
wahakikishe wanatekeleza majukumu yao kwa uadilifu.
Aidha Waziri Mkuu amewasisitiza watumishi wa
umma kufanya kazi kwa mujibu wa sheria kwa sababu vitendo vya wizi, uzembe
vinachangia kupunguza kasi ya kuwaletea maendeleo Watanzania.
Mbali na hilo Waziri Mkuu aliwataka Wakuu wa idara na watendaji wengine wa halmashauri kuacha tabia ya kukaa ofisini na badala yake waende vijijini kwa ajili ya kuwafuata wananchi na kushirikiana nao katika kutatua kero mbalimbali zinazowakabili.
Chanzo:Eatv
No comments:
Post a Comment