MPANDA
Wafanya biashara wa Zao la mahindi katika Soko la Mpanda
Hotel katika Halimashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wanakabiliwa na ukata wa
mitaji yao kutokana na mahindi mapya kuanza kuanza kuingia sokoni.
Wakizungumza na Mpanda Radio wamesema wateja wengi
wanapendelea kununua mahindi mapya ambayo yanauzwa kwa shilingi elf 36kwa gunia
tofauti na mahindi ya zamani yanayo uzwa shilingi elfu 42 kwa gunia.
Aidha wamebainisha changamoto wanazo kumbana nazo katika kazi
yao kuwa ni pamoja na baadhi ya wakulima kuwawadanganyifu wakati wa kununua
mazao hayo hususani suala la vipimo
Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa Mikoa inayo tajwa kuzalisha
kwa wingi mazao ya chakula hapa nchini ikiwemo Mahindi
Chanzo:Paul Mathius
No comments:
Post a Comment