KATAVI
Uhaba wa mabweni
katika shule za Sekondari Mkoani Katavi umetajwa kuchangia kushusha taaluma ya
wanafunzi hasa wa kike
Mpanda radio imetembelea
shule ya Sekondari Kabungu iliyopo wilaya ya Tanganyika, moja ya shule za
sekondari mkoani Katavi inayokumbana na changamoto hiyo
Baadhi ya wanafunzi wa
shule hiyo wamesema kukosenakana kwa mabweni katika shule za sekondari
kunasababisha wasome katika mazingira magumu na hata wengine kulazimika kuishi
kinyumba na wanaume
Mkuu wa shule hiyo
Mwalimu Patrick Kapita amesema shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 627 wa kidato
cha kwanza mpaka cha sita na kati ya hao
ni wanafunzi 52 pekee wa kidato cha kwanza hadi cha nne ndio wanaokaa hosteli
na wengine 128 wa kidato cha tano na sita
Kufuatia hali hiyo
uongozi wa shule ya sekondari Kabungu umepanga kukutana na wadau wa elimu siku
za usoni kujadili changamoto hiyo na kupanga ni namna gani ya kutatua
changamoto za kieleimu kwa wanafunzi
Chanzo: Haruna
No comments:
Post a Comment